Shy-Rose Bhanji akemea Ubaguzi wa Rangi uliooneshwa na Wana CCM Zanzibar

share on:

ccm ubaguzi machotara zanzibarJana ilikuwa ni kumbukumbu ya Sherehe za Mapinduzi Zanzibar ambapo iliudhuliwa na Raisi wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli.
Lakini kulionekana na Dosari kwenye moja kati ya picha ambayo imeonesha watu waliovalia jezi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo mmoja wao alishika bango lililoandikwa “MACHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA”
shy-rose Bhanji
Mbunge wa Afrika Mashariki Bi. Shy-Rose Bhanji ameoneshwa kukerwa na kitendo hicho na kupelekea kusema haya, “Say No to Racism: 52 years after the Zanzibar Revolution, racism has no place anymore. Whichever colour of your skin, you are a Zanzibari. United we stand, divided we fall.

Ikiwa ni miaka 52 baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, ubaguzi wa rangi hauna nafasi tena. Bila ya kujali rangi ya mtu, kila mtu ni Mzanzibari. Na hivo basi tukibaguana mwisho wake ni kutengana na tukiwa wamoja tutaimarisha Zanzibar” Akamalizia na #UmojaNiUshindi

Comments

comments

Leave a Response