Mpoto kuachia wimbo ‘Sizonje’ akiwa amemshirikisha Banana Zorro

share on:

Mpoto-na-Banana-wakisikiliza-walichokifanyaMpoto kuachia wimbo ‘Sizonje’ akiwa amemshirikisha Banana Zorro
Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia wimbo Jumatano hii anajipanga kuachia wimbo mpya uitwao ‘Sizonje’ akiwa amemshirikisha msanii kutoka B Band, Banana Zorro.
Akizungumza na mwandishi wetu Jumatatu hii, Mpoto alisema kazi hiyo iliyotayarishwa katika studio yake chini ya producer Allan Mapigo, ni kazi bora ambayo itakonga mioyo ya mashabiki wake.

“Nimefanya kazi ambayo kila mtu akiisikiliza atatoka na kitu chake kwa sababu ni kazi ambayo nimetumia muda mwingi kuiandaa,” alisema “Sizonje ambae namzunguzia kwenye hii nyimbo ni mtu, yaani hawa wewe kwenye kazi yako, nyumbani, hospitali unaweza ukawa Sizonje. Kwahiyo ni wimbo ambao kila mtu akiusikiliza atatoka na kitu,”,
Aliongeza “Hii kazi ni yule Mrisho Mpoto wa Nikipata Nauli, Kazi ambayo mpaka leo mtu akisikiliza anatamani zaidi kuendelea kusikiliza ili aelewe nini kinaendelea kwenye hii dunia,”.

Mrisho Mpoto na Banana Zoro waliwai kufanya kazi ya pamoja ya wimbo ‘Nikipata Nauli’ ambayo ilifanya vizuri.

Comments

comments

Leave a Response