Diamond Platnumz kajenga Msikiti wenye thamani zaidi ya Milioni 30

share on:

Inawezekana umemuona mwimbaji staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz akiwa kwenye maisha mazuri kuanzia nyumbani kwake mpaka usafiri anaotembelea ila hujajua kwamba amekua akifanya ibada na kumshukuru Mwenyenzi Mungu.

Diamond Amesema, “Msikiti nimeujenga kule Mkuyuni Morogoro ni baada ya boss wangu Tale kuniambia kwamba kuna msikiti kule Mkuyuni na watu wanaswali kwa tabu sababu Msikiti ni wa udongo, watu wanapata tabu.”

Diamond akaongezea, “Tuliuvunja mpaka tukaanza mwanzo kuujenga, sasa hivi ulipofikia ni karibia kukamilika…. gharama yake mpaka kukamilika ni zaidi ya milioni 30.”

Akaendelea, “Mwaka 2015 nilijitahidi kufanya vitu vingi vya dizaini hii Mwenyenzi Mungu aone kabisa inawezekana kazi yangu ya muziki sio nzuri ila natumia kufanya mambo ya msingi.”

KWA PICHA ZAIDI BONYEZA HAPA KUPATA APPLICATION YETU – DIAMOND HASSBABY APP

Comments

comments

Leave a Response