Tigo yawapa wateja wake huduma ya WhatsApp bure

share on:
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa  mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jana  Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam 
 Wafanyakazi wa Tigo na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakifurahia jambo  wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
 Hapa kila mgeni mualikwa akiwa busy na simu yake kwenye uzinduzi huo.
 Ni kama wanasema ‘tumependeza sana ngoja tujipige picha’  wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam


.
Wageni waaalikwa wakiwa katika maski za  ” Emojis “ wakifurahia jambo kwenye uzinduzi   huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
 Hapa ni furaha tupu kwa wanahabari.
 Washereheshaji katika uzinduzi huo,Mc  Taji Liundi na Mc Abby wakitoa maelezo jinsi gani wateja wa Tigo watakavyofurahia huduma ya whatsapp bure 
 Burudani ikiendelea kutoka kwa wasanii wa kikundi maalum cha maonesho ya jukwaa  wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini  Dar es salaam.
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez  (katikati), akiwa na viongozi wenzake kutoka tigo katika maski za “Emojis “ wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez  (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washereheshaji MC Taji Liundi na MC Abby  wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
 Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kushoto )  Meneja wa gharama  wa Tigo Jakhangic Tulaganov  na Meneja masoko Olivier prentout wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency 
Bloggers wakiwa katika picha ya pamoja na msanii Lucas  Muhuvile ‘Joti’  wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency 
Dar es Salaam, Februari 2, 2016– Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa
maisha ya kidijitali imetangaza huduma ya bure ya WhatsApp kwa watumiaji wa huduma
hiyo  ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni
ya simu  kutoa ofa ya bure  ya mtandao huo wa jamii  nchini.
 Akitangaza upatikanaji
bure wa huduma hiyo kwa vyombo vya habarijijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa
Tigo Diego Gutierrez amesema kuwa wateja wote wa Tigo  wanaotumia
vifurushi vya intaneti  vya
kampuni hiyo kwa wiki na mwezi  watapata huduma
ya WhatsApp bure. Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10.
Huduma ya WhatsApp ambayo ni maarufu kwenye kutuma
ujumbe  kwa njia ya simu, ina watumiaji
zaidi ya milioni nane nchini Tanzania
na  duniani  inatumiwa na watu wapatao milioni 900.
WhatsApp inawezesha watumiaji
kubadilishana habari, ujumbe, video na miito ya sauti.
“Kuanzia sasa na kuendelea wateja wote wa Tigo wanaonunua
vifurushi vyetu vya wiki au mwezi  watakuwa
na fursa ya kufurahia  WhatsApp BURE.
Hili linawezekana kama mteja ana smartphone. Huduma ya bure ya WhatsApp kwa
wateja wetu inaonesha  jinsi
tulivyojikita katika kuboresha mabadiliko kwenye  maisha ya kidijitali  na hivyo kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya
hali ya juu pamoja na ubunifu”, alisema Gutierrez.
Kwa Mujibu wa Gutierrez, ili kufurahia huduma hii, jambo
analohitaji mteja wa Tigo ni kuwa na
kifurushi cha intaneti  cha wiki
au mwezi  ambacho anaweza kukipata
kupitia *148*00# àTigo-Tigo Xtreme/MiniKabangà Wiki au Mwezi + WHATSAPP YA
BURE. Huduma hii inapatikana kwa wanaomiliki simu  za aina ya Blackberry, Android na Nokia Symbian60.

 

WhatsApp ni huduma dada na huduma huduma Facebook ambayo
iliingia makubaliano na Tigo mwaka 2014 na kuwapa fursa wateja wa Tigo huduma
ya Facebook bure na kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao.

Comments

comments

Leave a Response